Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SBL yaweka mkakati matumizi ya nishati safi ifikapo 2030

Mitungi Nya Gesi Bei.png SBL yaweka mkakati matumizi ya nishati safi ifikapo 2030

Fri, 26 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya nishati safi, Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL), sehemu ya makampuni ya Diageo, imeweka mkakati wa utekelezaji wa matumizi ya nishati safi hadi kufikia 2030.

Dira hiyo yenye kaulimbiu ya ‘Dunia iliyo safi’ inaendana na mpango mkakati wa miaka 10 wa Diageo katika matumizi ya nishati hiyo.

Taarifa ya SBL iliyotolewa leo Jumatano, Januari 25, 2024 inasema kwenye masuala ya utawala, mazingira na ya kijamii, kampuni hiyo imeendelea kupiga hatua kuelekea kupunguza athari za mazingira na kuweka mkakati wa suluhisho la upatikanaji wa nishati safi.

"Katika mpango mkakati wa miaka 10 wa Diageo kwenye masuala ya utawala, mazingira na kijamii katika kuelekea kupunguza athari za mazingira, tumeweka mkakati wa kuondokana na taka na kuboresha ufanisi.

"Kwa miaka mitano iliyopita, kampuni imefanikiwa kupunguza zaidi ya nusu ya matumizi ya nishati na maji. Umuhimu wa awamu hii unaonekana kwenye manufaa ya haraka katika uhifadhi wa rasilimali na ufanisi katika uendeshaji,” imeeleza taarifa hiyo.

Ilibanisha katika michakato yake ya uzalishaji wa vilevi, uunganishwa wa mifumo ya kurejesha nishati sio tu unapunguza athari ya kiikolojia, lakini pia unadhibiti joto wakati wa mchakato wa uchanganyaji wa kimea.

Taarifa hiyo imeeleza ufundi na unyumbilikaji huo baina ya shayiri iliyochanganywa na maji ya moto, huachilia sukari, rangi na ladha, ambazo huchukua nafasi ya kutengeneza mvuto endelevu unaoendana na mazingira.

Hivyo, SBL inaeleza safari ya kuelekea kwenye matumizi ya nishati ya jua imeanza kupitia tathmini yao waliyoifanya na watoa huduma wengine.

“Umuhimu wa uwekezaji huu hauwezi kupuuzwa, nishati endelevu itokanayo na mimea asilia na jua, huwakilisha mabadiliko kuelekea njia mbadala safi zaidi ya kupunguza kiwango cha kaboni kinachozalishwa na kampuni huku ikichangia mabadiliko kwa vyanzo vya nishati mbadala," imeeleza taarifa hiyo ya SBL.

Imesema kampuni hiyo inapobadilisha mifumo ya matumizi ya nishati, sio tu inajitengenezea mustakabali endelevu zaidi, lakini pia inaweka mfano bora kwa wadau wengine katika sekta kufuata nyayo.

Akizungumzia nishati safi ya kupikia leo akiwa nchini Indonesia, Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania inafanikiwa katika matumizi ya nishati safi hususan ya kupikia. Amesema Serikali itatumia uzoefu kutoka taifa la Indonesia kuhusiana na nishati hiyo.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa nchi, Indonesia ni miongoni mwa mataifa yaliyofanikiwa katika matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Mwaka jana, Rais Samia alizindua mpango wa matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini, akilenga kile alichoeleza, kupunguza athari za matumizi ya nishati isiyofaa.

Akizungumza leo Januari 25, 2024 akiwa Ikulu ya Bogor nchini Indonesia, Rais Samia amewaambia waandishi wa habari kuwa, Serikali yake itatumia uzoefu wa Indonesia, ili kufanikiwa kwenye mpango wa matumizi ya nishati safi ya kupikia.

"Kwa sababu Indonesia imefanikiwa katika matumizi ya nishati safi ya kupikia, nitashirikiana nayo kuhakikisha Tanzania inapata ujuzi na uzoefu," amesema.

Sambamba na hilo, Rais Samia ameikaribisha Indonesia kuwekeza katika sekta ya nishati jadidifu nchini Tanzania, akisema ni eneo lenye fursa nyingi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live