Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SBL yapanua sasa viwanda vyake

SBL BREW Kiwanda cha Beer

Wed, 15 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

LICHA ya vikwazo kwa biashara nyingi duniani kutokana na ugonjwa wa corona, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imesema kusimama imara na kuendelea katika uzalishaji.

Kampuni hiyo imesema imeweza kukamilisha upanuzi wa kiwanda chake cha bia cha Dar es Salaam uliogharimu paundi za Uingereza milioni 10 (sawa na shilingi bilioni 30), huku upanuzi wa kiwanda chake cha Moshi ukiwa unaendelea kwa gharama ya Paundi za Uingereza milioni 4.5 (sawa na Shilingi bilioni 13.5).

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti, uwekezaji huo mkubwa umechangiwa kwa kiasi kikubwa na mazingira mazuri ya biashara ambayo pia yamesababisha kukua kwa soko la bia nchini.

“Tulitoa ahadi kwa wateja wetu kuwa kama mahitaji yataongezeka, tutawekeza katika kupanua uzalishaji ndani ya miaka michache ijayo na ndicho ambacho tumekifanya na tunachoendelea kukifanya,” Ocitti alisema.

Alisema upanuzi huo wa uzalishaji umekwenda sambamba na ongezeko la kodi ambalo kampuni hiyo imelipa kwa Serikali. Mwaka jana SBL ililipa shilingi bilioni 132 kama kodi ikiwa ni ongezeko la asilimia 10 kutoka shilingi bilioni 121 iliyolipwa mwaka 2018.

Ukuaji wa kampuni hiyo kwa mujibu wa mkurugenzi wake mtendaji, umewezesha kuongezeka kwa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja ambapo kwa sasa zaidi ya watu 800 wameajiriwa na kampuni hiyo.

Alisema wakulima wanaozalisha shayiri, mtama na mahindi mazao ambayo hutumiwa na kampuni hiyo kuzalisha bia ni kundi lingine ambalo linanufaika na upanuzi. SBL ilinunua zaidi ya tani za ujazo 17,000 za nafaka kutoka kwa wakulima wa ndani sawa na asilimia 70 ya mahitaji yake yote ya malighafi katika kipindi cha mwaka jana.

“Lengo letu ni kuongeza kiasi cha malighafi tunazonunua kutoka kwa wakulima wa ndani na kufikia asilimia 85 ya kiwango kinachotakiwa kwa uzalishaji wa bia kufikia mwaka 2022, jambo ambalo litawahakikishia wakulima uhakika wa soko kwa mazao yao,” aliongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live