Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SBL yamwaga Sh.Bilioni 2 kwa baa kupambana na corona

1 (7) SBL yamwaga Sh.Bilioni 2 kwa baa kupambana na corona

Thu, 1 Jul 2021 Chanzo: ippmedia.com

Msaada huo wa SBL unakuja wakati dunia ikipambana na wimbi la tatu la ugonjwa wa corona huku nchi mbalimbali zikiendelea kuwakinga raia wake ili kuhakikisha shughuli za kiuchumi zinaendelea kama kawaida.

 

Programu hiyo ya SBL, inajulikana kama “Raise the Bar” au “Tunyanyuke Pamoja”, itadumu kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia Julai 2021 na baa zitapata misaada ya vifaa na mafunzo baada ya kujiandikisha na kukidhi vigezo maalumu kupitia tovuti ya www.diageobaracademy.com.

 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti, amesema mpango huo wa SBL ni mchango wa kampuni hiyo katika kuunga mkono jitihada za serikali kuwahamasisha watu na biashara kuweka mazingira safi ili kujikinga na magonjwa ya kuambukiza ikiwamo ugonjwa wa corona.

 

“Katika programu hii, tutazisaidia baa kuwa na mazingira safi na salama ili kuweza kuwalinda wateja wanaopata huduma ya chakula na vinywaji dhidi ya magonjwa mbalimbali kiwamo ugonjwa wa corona. Lengo letu ni kuyafanya yanyanyuke tena. Programu hii itazinufaisha baa zaidi ya 2,000 katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha pamoja na Zanzibar,” amesema

 

Programu hiyo ni sehemu ya kampeni ya kidunia inayofadhiliwa na kampuni mama ya Serengeti, Diageo unaolenga kusaidia mabaa kupambana na ugonjwa wa UVIKO19. Miji mingine inayonufaika na mradi ni pamoja na Nairobi, Kampala, New York, London, Edinburgh, Dublin, Belfast, Mexico City, Sao Paulo, Shanghai, Delhi, Mumbai, Bangalore, Sydney.

 

Kwa mujibu wa Diageo, programu ya“Raise the Bar” au “Tunyanyuke Pamoja” ilibuniwa baada ya utafiti uliofanywa kwa wenye baa wakitafuta namna ya kuyasaidia kurudi kwenye biashara wakati wa kipindi cha corona. Vipaumbele vilivyobainishwa ni pamoja na masuala ya usafi wa mazingira, misaada ya namna ya kufanya biashara kwa kuchukua tahadhari na vifaa vitakavyosaidia kujikinga.

 

“Raise the Bar au Tunyanyuke Pamoja, itazisaidia baa kwa kuzipatia wafanyakazi wake uwezo zaidi wa kujikinga na magonjwa ya kuambukiza ikiwamo corona na pia itatoa vifaa mbalimbali kama meza, viti, vitakasa mikono na vifaa vingine kulingana na mazingira ya baa husika. Lengo ni kuwahakikishia wateja usalama wa afya zao pindi wanapofika kupata huduma ya vinywaji au chakula,” amesema Ocitti.

Programu hiyo ipo wazi kwa baa zote kubwa na ndogo zilizosajiliwa na ambazo zina leseni ya kuuza pombe katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Zanzibar. Ili baa iweze kufikiriwa kupata msaada chini ya programu hii, ni lazima iwe ikifanya biashara walau mwaka mmoja kabla ya corona kuingia hapa nchini.

Dirisha la maombi tayari limeshafunguliwa baa ili muweze kupata msaada, yanatakiwa kutembelea tovuti ya Diageo Bar Academy www.diageobaracademy.com na kujisajili. Wawakilishi was SBL watakuwa wakipita katika baa kwa ajili ya kuwaelekeza na kuwasaidia kuzisajili baa zenu.

“Serengeti ikiwa kama mdau wa baishara hapa nchini inapenda kuzisisitiza baa zote zenye sifa katika mikoa niliyoitaja kuchangamkia fursa hii,” amesema 

Chanzo: ippmedia.com