Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SADCAS yathibitisha uwepo wa maabara nne TBS

Large 1650863845 Tbslogo.png SADCAS yathibitisha uwepo wa maabara nne TBS

Fri, 26 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TAASISI ya Ithibati ya Jumuiya ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADCAS) imethibitisha na kuzipatia vyeti vya umahiri maabara nane za Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Akizungumza Januari 25, 2024 jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Ithibati ya Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADCAS), Eva Christine Gadzikwa amesema vyeti hivyo vya umahiri vilivyotolewa na hatua nzuri kwa Tanzania ambayo inathihirisha kuwa maabara hizo zinaendelea kukubalika popote duniani jambo linaongeza chachu katika uwezeshaji biashara ndani na nje ya nchi.

Amesema, maabara hizo nane zitaendelea kusaidia na kurahisisha biashara kwani majibu ya maabara hizo yataweza kukubalika na kutumika popote duniani. - "Hakuna haja tena ya kupima bidhaa zilizoidhinishwa hapa Tanzania zitakaposafirishwa nje ya nchi ambapo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuokoa muda na kulinda wateja". Amesema Christine

Ne, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) David Ndibalema amesema kuwa wanafuraha kubwa ya kupokea vyeti vya umahiri ambavyo vitasaidia kutambulika kimataifa kwa huduma zinazotolewa na shirika hilo, itasaidia bidhaa zinazozalishwa nchini kuingia katika ushindani kwenye masoko ya nje na ndani ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live