Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruvuma yazalisha ziada mazao ya chakula

2baf3f0c4de6449788949fc688ef91b2.jpeg Ruvuma yazalisha ziada mazao ya chakula

Sun, 2 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kuvuna tani 1,384,705 za mazao ya chakula katika msimu wa kilimo 2020/2021, huku mahitaji ya chakula kwa wakazi wa mkoa huo ni tani 470,000 hivyo kuwa na ziada ya tani 914,705.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Wilbert Ibuge alisema hayo mwishoni jana, wakati akizungumza na wataalamu wa idara na taasisi mbalimbali za serikali katika kikao kazi kilichofanyika mjini Songea.

Alisema kutokana na uzalishaji huo, Mkoa wa Ruvuma umeendelea kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika uzalishaji wa mazao ya chakula kwa mara ya tatu mfululizo na kuwapongeza wakulima kwa jitihada kubwa wa-

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima (kulia) akiteta na Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Tanga, Upendo Lugongo (katikati) kabla ya hafla ya kusaini mikataba 16 ya miradi ya maji ya jumla ya Sh bilioni 8.1. Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Pili Mnyema. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa).

nazofanya katika uzalishaji mashambani.

Aidha alisema kwa upande wa zao la mahindi wakulima waliuza mahindi yao kupitia soko la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula(NFRA) baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutoa Sh bilioni 50 kwa ajili ya kununua mahindi ikiwemo Mkoa wa Ruvuma.

Alisema mkoa utaendelea kusimamia mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umeonesha mafanikio makubwa, ambapo katika msimu 2020/2021 zao la ufuta kilo 8,326,686 ziliuzwa kati ya bei ya Sh 1,998 na 2,393 kwa kilo na kuwaingizia wakulima Sh bilioni 17,221,852,087.

Mkuu wa mkoa alitaja mazao mengine ni soya ambayo iliuzwa kilo 1,090,199 na Sh 1,547,202,688 zilipatikana na huku zao la mbaazi nalo likionesha mafanikio makubwa ambapo kwa mara ya kwanza wakulima

wa mkoa huo waliuza jumla ya kilo 7,109,360 kwa bei ya Sh 1,428 na 990 na kuwapatia wakulima Sh 9,313,114,073.

Kwa mujibu wa Ibuge, mafanikio ya uzalishaji yanatokana na matumizi bora ya pembejeo za kilimo ambapo serikali inaendelea kuhamasisha wakulima kutumia mbolea mbadala kuliko walizozoea ambazo bei zake ziko juu.

Katika kuendeleza shughuli za kilimo Mkuu wa mkoa alieleza kuwa mkoa umeandaa mpango wa utekelezaji wa shughuli za kilimo kwa pamoja na kilimo cha mkataba katika msimu wa kilimo 2021/2022 na mpango huo utahusisha mazao ya alizeti,soya na ufuta.

Alisema lengo la mpango huo ni kuwaongezea tija na kipato wakulima kupitia mazao yanayouzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani na tayari mkoa

umeshatambua maeneo yanayofaa kwa kilimo hicho ambapo jumla ya ekari 48,343.35 zimetengwa katika halmashauri zote nane.

Hata hivyo alisema mafanikio ya shughuli za kilimo kwa sasa yanategemea sana mvua ambazo mwaka huu imeshaelezwa zitakuwa chache, kwa hiyo amewakumbusha wakulima kupanda mazao mara tu mvua zitakapoanza kunyesha na kupanda mazao ya muda mfupi yasiyohitaji mvua nyingi.

Katika hatua nyingine, Ibuge amewakumbusha watendaji na watumishi wa umma umuhimu wa kusimamia mapato yatokanayo na kodi pamoja na ushuru kuwa kazi hiyo ni ya kila mmoja kwani fedha zinazopatikana zinatumika kujenga miradi ya maende-

leo ikiwemo vituo vya afya,barabara,ununuzi wa ndege na ujenzi wa reli.

Ibuge amewapongeza wakurugenzi watendaji wa mamlaka za serikali za mitaa kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ambapo halmashauri zote zilikusanya mapato vizuri na kufanya mkoa kukusanya jumla ya Sh 16,984,706,090 kati ya lengo la kukusanya Sh 16,365,090,734.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho, amewapongeza watumishi wa ngazi mbalimbali kwa kutekeleza vyema majukumu yao jambo lililoufanya mkoa huo kuendelea kufanya vizuri katika maendeleo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live