Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Russia, Quatar zinavyoachana na dola...

Dola Dola Dola Russia, Quatar zinavyoachana na dola...

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika muendelezo wa sera ya kufuta sarafu ya dola katika miamala ya kibiashara kati ya nchi mbalimbali, Qatar pia imeondoa matumizi ya dola katika mabadilishano yake ya kibiashara na Russia, ambapo biashara baina ya nchi hizo mbili, sasa itafanyika kwa kutumia sarafu za taifa.

Kuhusiana na suala hilo, balozi wa Russia nchini Qatar Dmitry Dogadkin amesema: mabadilisihano ya kibiashara kati ya nchi mbili yanaendelea kustawi na kila upande unajaribu kuhakikisha unatumia sarafu yake ya taifa badala ya dola.

Dogadkin amefafanua kuwa, ushirikiano kati ya Moscow na Doha katika nyanja ya uwekezaji unaendelea kupanuka, na biashara baina ya pande hizo mbili katika robo ya kwanza ya 2023 imefikia zaidi ya dola milioni 19. Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin (kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Mohammad bin Abdulrahman Al Thani

Suala la kutumia ruble ya Russia na riali ya Qatar katika biashara kati ya nchi hizo mbili lilijadiliwa katika mkutano kati ya Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Mohammad bin Abdulrahman Al Thani mwezi Juni, na sasa imefikiwa hatua ya utekelezaji wake.

Russia, kwa kushirikiana na nchi nyingine nyingi duniani ilishaanza muda mrefu kuchukua hatua za kupunguza utegemezi wa dola katika miamala ya kibiashara. Hakika sera za mashinikizo ya juu kabisa za Marekani kwa nchi zisizofuata sera zake na utumiaji vikwazo vya kiuchumi dhidi ya nchi hizo umezifanya nchi nyingi ziamue kutumia sarafu nyingine kama vile ruble na yuan katika miamala ya kibiashara baina ya pande mbili.

Ukweli ni kwamba, hatua ya Marekani ya kuitumia sarafu ya dola kama silaha, siku zote imekuwa moja ya matatizo na vizuizi vikubwa vinavyokwamisha ustawi wa uuzaji bidhaa nje na miamala ya kimataifa kati ya nchi zisizofuata sera za Washington. Katika miezi ya hivi karibuni, sambamba na kuzuka vita kati ya Russia na Ukraine na kushadidishwa vikwazo dhidi ya Moscow, sera hiyo ya kuachana na sarafu ya dola imekuwa ikipewa uzito mkubwa zaidi na Russia, China na washirika wao wa kibiashara. Kwa hakika, kutumiwa dola na Marekani kama silaha ya kifedha kumeongeza kiwango cha kukubalika na kueleweka udharura wa kutumia aina nyingine ya uwekezaji kupitia sarafu mbadala miongoni mwa nchi mbalimbali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live