Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruksa kusajili laini zaidi ya moja

53688 Pic+laini

Tue, 23 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Watanzania wamepewa ufafanuzi kuhusu matumizi ya laini za simu kuwa hakuna zuio la kutumia laini zaidi ya moja.

Hata hivyo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amesema ni muhimu kuondoa utitiri wa laini za simu.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Rombo (Chadema) Joseph Selasini leo Jumanne Aprili 23, 2019 aliyetaka kujua kuhusu uvumi kwamba usajili mpya wa laini za simu unamtaka kila Mtanzania kumiliki laini moja.

“Ni kweli kuwa nimekuwa nikirudia kuzungumza jambo hili mara kwa mara, kuanzia Mei tutaanza kusajili laini zetu kupitia alama za vidole, lakini si kwamba tunazuia laini za simu bali kuna laini za hovyo hovyo zinazowasumbua kuwa mtume fedha," amesema Nditiye.

Amesema kikubwa kinachoangaliwa ni kuona kama Serikali inaweza kupunguza utitiri ikiwemo baadhi ya watu kuwa na laini zaidi ya moja katika mtandao mmoja lakini kuwa na mitandao mingine haina shida.

Naibu Waziri huyo amesema kwamba utaratibu wa kusajili laini hautakuwa na madhara badala yake usalama zaidi ndio unaoangaliwa



Chanzo: mwananchi.co.tz