Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rolls Royce kupunguza wafanyakazi 2,500

ROLLS ROYCE (600 X 339) Rolls Royce kupunguza wafanyakazi 2,500

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KAMPUNI ya Rolls Royce imeamua kupunguza wafanyakazi 2,500 katika kile inachoita kutafuta ufanisi wa kimataifa, kampuni hiyo yenye makao yake Uingereza imetangaza rasmi.

Kampuni hiyo inayohusika na mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mifumo ya ulinzi na anga, imesema kwamba inataka kutengeneza mazingira sahihi na rahisi zaidi. Kampuni hiyo yenye makao makuu Derby, kwa sasa imeajiri watu 42,000 katika nchi mbalimbali.

Kadhalika, kampuni hiyo imeeleza mipango yake ya kuuganisha timu zake zinazoshughulikia teknolojia ya uhandisi na ile ya usalama kuwa moja, itakayokuwa na wajibu wa usalama wa bidhaa, viwango vya uhandisi, michakato, njia na zana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live