Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Repoa: Tanzania hainufaiki ipasavyo na sekta ya uziduaji

Repoa Pic Tanzania hainufaiki ipasavyo na sekta ya uziduaji

Mon, 1 Aug 2022 Chanzo: Mwananchi

Licha ya utajiri wa rasilimali za asili (madini, mafuta na gesi) uliopo Tanzania, Taasisi ya Utafiti Repoa imesema bado nchi hiyo hainufaiki ipasavyo na sekta hiyo.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu, Agosti Mosi, 2022 na Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa, Dk Donald Mmari, wakati wa semina kwa wadau wa sekta ya uziduaji (mafuta, gesi na madini).

Amesema uzalishaji katika sekta hiyo hutegemea uwekezaji mkubwa wa rasilimali fedha na teknolojia, jambo ambalo Tanzania haijafanya vya kutosha.

"Nchi yetu bado hatujajenga uwezo sana kwa maana ya kiteknolojia na fedha zinazoweza kuwekezwa katika miradi kama hii," amesema.

Kwa mujibu wa Dk Mmari, uwekezaji katika miradi hiyo sio wa uhakika kwamba utazalisha kama unavyotarajia hivyo, kinahitajika uwezo mkubwa wa kiuchumi kufanikisha hilo.

Amesema lazima wawekezaji binafsi washirikishwe ili kufanikisha uwekezaji katika sekta hiyo.

Chanzo: Mwananchi