Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais azindua kiwanda cha maparachichi

54696 Parachici+pic

Tue, 30 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amezindua kiwanda cha maparachichi cha Rungwe Avocado Company Limited (RACL)  chenye uwezo wa kuhudumia wakulima wa zao hilo 20,000 na kutoa ajira za moja kwa moja 135.

Mbali na kufungua kiwanda hicho, Rais pia ameahidi  kushughulikia urejeshwaji wa ‘VAT refund’ kwa wawekezaji ili waweze kutumia pesa zao katika kufanya shughuli nyingine.

Ameyasema hayo leo Aprili 29, 2019 baada ya kuzindua kiwanda hicho ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoani Mbeya.

Magufuli amesema wamiliki wa kiwanda hicho wanapaswa kutoa bei nzuri ya maparachichi kwa wakulima ili waweze kunufaika na kile wanachokizalisha na kufurahia uwepo wake.

“Wakati Serikali inashughulikia matatizo yenu na nyie toeni bei nzuri kwa wakulima na wafanyakazi wenu muwape mshahara mzuri ili waweze kufanya vitu vyao vizuri,” amesema Magufuli.

Akizungumzia urejeshwaji  wa VAT kwa wawekezaji na wafanyabiashara alisema umekuwa na matatizo kutokana na wao kuongeza gharama kwa vitu wanavyonunua ili wapate fedha nyingi kutoka serikalini.

“kulikuwa kukifanyika ‘Vat refund’ hewa mtu amenunua vifaa vya Sh5 milioni anasema alinunua Sh50 milioni, tumelaliwa sana katika kipindi cha nyuma ndiyo maana serikali kupitia wizara ya Fedha ikasema lazima ikague ‘VAT refund’ zote kabla ya kufanyika malipo,” amesema Magufuli

“Kama ambavyo wanafanya katika nchi nyingine kabla ya kulipa lazima wathibitishe uhalali wa pesa mnazodai ninawahakikishia kuwa mtalipwa, ila mlete madai halali msiongeze na ikiwezekana mpunguze,”



Chanzo: mwananchi.co.tz