Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais ateta na Wafanyabiashara hali ya chakula na bei

FB IMG 1676211551017 1080x640 Rais ateta na Wafanyabiashara hali ya chakula na bei

Sun, 12 Feb 2023 Chanzo: Dar 24

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewatembelea wafanyabiashara mbalimbali wa maduka ya vyakula ya rejareja.

Ziara hiyo ya kushtukiza, ilikuwa na lengo la kujionea hali ya chakula ilivyo na bei zake katika eneo la Chake Chake Pemba hii leo Februari 12, 2023.

Aidha, Rais Mwinyi pia alipata wasaa wa kupokea maelezo kutoka kwa wafanyabishara hao, kuhusiana na bei za vyakula na upatikanaji wake.

Chanzo: Dar 24