Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia kufungua Maonesho Sabasaba leo

38441bb3ed8d8cfa7b0a7ab847679f37 Rais Samia kufungua Maonesho Sabasaba leo

Mon, 5 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS Samia Suluhu Hassan leo atafungua Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba katika viwanja Maonesho vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Ofisa Habari wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade), Daniel Diah alilieza HabariLEO jana kuwa, Rais Samia atafungua maonesho hayo kama ilivyoelezwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo alipozungumza na waandishi wa habari Juni 28, mwaka huu.

Profesa Mkumbo alisema Rais Samia ameridhia kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi huo leo.

Kwa mujibu wa Profesa Mkumbo, kiingilio katika maonesho hayo ni Sh 3,000 kwa mtu mzima na Julai 7 itakuwa Sh 4,000 na kwa watoto ni Sh 1,000.

Kauli mbiu ya maonesho hayo mwaka huu ni ‘Uchumi wa Viwanda kwa Ajira Endelevu.’

Mwaka huu washiriki wa jumla wameongezeka kwa takribani 800 kutoka 2,880 mwaka jana hadi 3002 mwaka huu, huku nchi zaidi ya 15 zikishiriki, kampuni za kigeni 76 kutoka 43 zilizoshiriki mwaka jana.

Hata hivyo, pamoja na ongezeko hilo la washiriki, serikali imeendelea kukazia watu kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Miongoni mwa tahadhari hizo ni kabla ya kuingia ndani, kila mtu kupimwa joto la mwili, kuvaa barakoa na kunawa mikono kwa maji tiririka yaliowekwa nje ya milango ya kuingia.

Chanzo: www.habarileo.co.tz