Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia aagiza kutengwa hekari 100,000 kilimo cha alizeti

Samia Makazii Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Thu, 9 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa Mkoa wa Kagera kutenga ardhi kati ya hekari elfu 70 hadi laki moja kwa ajili ya kulima mashamba makubwa ya alizeti pamoja na michikichi ili kuondoa utegemezi wa mafuta hayo kutoka nje ya nchi.

Rais Samia Hassan ameyasema hayo leo Juni 09, 2022 wakati akiwa katika Kiwanda cha Kagera Sukari kilichopo Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera wakati akiongea na wafanyakazi wa kiwanda hicho baada ya kukagua mashamba yanayozalisha miwa.

"Tanzania tumekuwa tukitegemea mafuta ya kula kutoka nje lakini kutokana na janga la Uviko-19 tumepata tatizo la kukosa mafuta baada ya kufungwa mipaka hivyo hatuna budi kufanya uzalishaji wa ndani na ili tujitosheleze lazima tuwe na mashamba makubwa ya alizeti pamoja na michikichi,"amesema Rais Samia.

Amesema Kagera ni mkoa wa mwisho kiuchumi  na una ardhi kubwa ya kutosha lakini haitumiki.

Amesema kama Serikali wamekuja na sera ya kilimo cha mashamba makubwa ambapo kiasi cha Sh20 bilioni kitatumika kuendeleza mashamba hayo makubwa kwa ajili ya kilimo cha alizeti na michikichi.

Ameongeza kwamba, nchi ya Tanzania ni kubwa wakitegemea mafuta ya nje watakwama na hivyo lazima wajikite kwenye kilimo cha mazao ya kuzalisha mafuta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live