Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia: Biashara zetu bado ziko chini ya 15%

959e75f0dec87ce2bb3ed16c13e19eed.png Rais Samia Suluhu Hassan

Sat, 23 Jul 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS Samia Suluhu, amesema biashara za nchi Jumuiya ya Afrika Mashariki bado zipo chini ya asilimia 15 na kutaka hatua zaidi zichukuliwe ili kukuza biashara.

Akizungumza jana Julai 22, 2022, Rais Samia amesema hakuna hatua za kutosha zilizochukuliwa ili kukuza biashara ndani ya jumuiya hiyo.

“Bado tunazungumzia kuondoa vikwazo vya kikodi vilivyosalia, na hii inatokea biashara ya nchi zetu zipo chini ya asilimia 15 hii inaonyesha hatufanyi hatua za kutosha katika kuboresha utendaji katika kukuza uchumi wa forodha.”Amesema Rais Samia na kuongeza

“Tufikirie hili suala kwa maana nyingine sera zetu na mifumo tunayoweka, vinalenga kurahisisha biashara na nchi nyingine nchi za jumuiya na kutubana wenyewe kuhusu fursa.”Amesema

Aidha, Rais Samia ametoa changamoto kwa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya kutizama jitihada ambazo zitaweza kuchukuliwa ili kuondoa tatizo hilo.

“Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ni sehemu ya ukanda huru wa biashara katika sehemu ya Afrika, kama hatuko makini kuangalia jumuiya yetu inanufaika na si nchi moja moja, tutakuwa tunawasaidia tu wengine.

“Lazima tukumbuke wakati wote waliolala watachukuliwa na upepo kuelekea wasipopajua kwa hiyo tusiwe sisi, tusikubali kuchukuliwa, Baraza la Mawaziri lazima liweke kipaumbele kwenye masuala yaliyopo katika mnyororo wa thamani, kuongeza biashara ya mipakani na uwekezaji, hii itatusaidia, kuwezesha imani kwa watu wetu na kuwafanya waweze kumiliki mchakato wa mtangamano.” Amesema

Chanzo: www.habarileo.co.tz