Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Mwinyi aanika mikakati kutatua changamoto za vijana katika kilimo

Rais Mwinyi Asifu Miaka 59 Ya Muungano .jpeg Rais Mwinyi aanika mikakati kutatua changamoto za vijana katika kilimo

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema pamoja na utashi uliopo wa kuwahusisha vijana katika shughuli za kilimo-biashara, bado inahitajika mikakati zaidi ya kukabiliana na changamto zinazowakwamisha.

Kauli ya Rais Mwinyi ameitoa kauli hiyo leo Alhamisi Septemba 7, 2023 alipokuwa akihutubia katika Jukwaa la Mifumo ya Chakula (AGRF) linalofanyika jijini hapa.

Amesema pamoja na juhudi zinazofanywa kimataifa na kitaifa za kuwasaidia vijana, bado wanakabiliwa na changamoto.

“Bado kuna ushiriki mdogo wa vijana na wanawake katika sekta za kilimo na uvuvi zinazotokana na changamoto mbalimbali zikiwemo upatikanaji mdogo wa rasilimali za uzalishaji; ujuzi mdogo wa ujasiriamali katika kilimo; vizuizi katika mgawanyo wa rasilimali pamoja na ugumu wa upatikanaji wa mitaji katika kuendeleza ujasiriamali wao,” amesema.

Amesema kutokana na kukua kwa mifumo ya kidijitali inayosimamia mabadiliko ya uchumi wa kidunia, kumekuwa na ongezeko la kasi la vijana kujishughulisha na kuwa sehemu ya uchumi wa Afrika.

“Vijana wanayo hamu ya kuwekeza pale ambapo wataweza kupata faida ya haraka katika sekta ya kilimo na uvuvi,” amesema.

Ametaja maeneo yaayotakiwa kupatiwa ufumbuzi kuwa pamoja huduma za kijamii katika maeneo ya vijijini kunakosababisha kuwepo na ongezeko la wimbi la vijana kukimbilia mijini; uwepo wa changamoto nyingi katika upatikanaji wa uzalishaji na masoko, vikwazo vya kimazingira na mabadiliko ya tabianchi.

“Pia mara nyingi kuwepo kwa faida ndogo inayotokana na uwekezaji kinyume na matarajio ya vijana, upatikanaji mdogo wa mitaji na masoko, kukosekana kwa miundombinu ya uzalishaji na usafirishaji wa mazao pamoja na kukosekana kwa teknolojia ya kisasa,” amesema.

Amesema Zanzibar ina mfano mahsusi wa namna Serikali inavyoshirikiana na taasisi za kifedha katika kutatua mahitaji ya mitaji ya wajasiriamali katika utekelezaji wa Uchumi wa Buluu.

Akizungumza awali, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe alisema wakati idadi ya Watanzania ikiendelea kukua kwa kasi, mikakati inawekwa zaidi kwa vijana kwa kuwashirikisha katika mfumo mzima wa uzalishaji.

“Hatuzungumzii tu kilimo, hatuzungumzii tu ufugaji, au uvuvi, tunazungumzia mfumo mzima wa uzalishaji, usindikaji, kwenda sokoni hadi kwenye matumizi,” amesema.

Amesema katika kutumiza ndoto ya kuifanya Tanzania kuwa kapu la chakula la Afrika programu za vijana katika kilimo ndio zinazingatia katika mnyororo wa kilimo.

“Programu ya Jenga Kesho iliyo bora (BBT), inalenga katika mnyororo wa uzalishaji. Kama tunavyojua vijana hawana uvumilivu, huwezi kumwambia akalime, aanzishe shamba la korosho leo asubiri miaka mitatu hadi mitano ndipo apate hela, watakimbia wote.

“Ndiyo maana tumeamua kuweka mazao yenye thamani kubwa kama mazao ya mbogamboga, mafuta ya kupikia, mifugo na uvuvi,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live