Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Magufuli aagiza maboresho ya nembo Kiwanda cha Mpunga

Bd1394ccd992504d53a51bd1c39470fb Rais Magufuli aagiza maboresho ya nembo Kiwanda cha Mpunga

Sat, 13 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Rais Dk John Magufuli amekitaka Kiwanda cha Mpunga cha Murzar Wilmar kilichopo mkoani Morogoro kutengeneza nembo nyingine katika mojawapo ya bidhaa inazozalisha kuwa na jina linalohusu Tanzania kama njia mojawapo ya kuitangaza nchi yetu.

Dk Magufuli amebainisha hayo leo Ijumaa alipokuwa anazindua kuwanda hicho mkoani humo chenye uwezo wa kukoboa tani 280 za Mpunga kwa siku.

“Sasa kwasababu mchele huu umetoka kwa wakulima kutoka Tanzania siwazuii kuendelea kuendelea kutumia nembo yenu ya Korie lakini pawe na ‘Brand’ nyingine inayotangaza Tanzania hiyo itakuwa njia mojawapo ya kuitangazaa nchi yetu” amesema Dk Magufuli.

Dk Magufuli amesema kuna bidhaa nyingi zenye ubora zinatoka hapa nchini yakiwemo maparachichi na nyama lakini zimebandikwa nembo kutoka nchi nyingine kitu kinachorudisha nyuma nchi yetu kujitangaza kwenye suala la uzalishaji.

Chanzo: habarileo.co.tz