Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raawu yataka nyongeza mishahara sekta binafsi

Pic Fedha Data Wastaafu Raawu yataka nyongeza mishahara sekta binafsi

Mon, 16 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Utafiti, stadi za ufundi na kazi nyinginezo (Raawu) kimemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuigeukie sekta binafsi katika nyongeza ya mishahara kwani sekta hiyo haijafanyiwa mabadiliko yoyote kwa miaka tisa.

Kwa mujibu wa Raawu waraka wa nyongeza za mishahara katika sekta binafsi ulitolewa kwa mara ya mwisho mwaka 2013.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu, Mei 16, 2022 na Mwenyekiti wa Raawu Taifa, Jane Mihanji alipokuwa akitoa pongezi kwa hatua ya Serikali kuongeza mishahara ya kima cha chini kwa asilimia 23.3.

“Tunamuomba Rais Samia kuiangalia pia sekta binafsi ambayo imeachwa pasipo kuguswa tangu ambapo waraka wa mwisho wa mishahara katika sekta hiyo uliotolewa mwaka 2013.

“Kwa kuwa bodi ya kima cha chini cha misharaha katika sekta binafsi imekwishaundwa tunaiomba Serikali ihakikishe bodi hii pia inatangaza mishahara katika sekta binafsi mapema iwezekanavyo,” amesema Mihanji.

Raawu inawasihi wafanyakazi wote katika sekta ya umma na binafsi kuongeza bidii katika utendaji kazi ili kuijengea uwezo Serikali kutokana na tija itakayopatikana na kumdhihirishia Rais kuwa nyongeza hiyo ya mishahara aliyowapatia watumishi wa umma imekuwa na faida pia kwa Serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live