Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RPOTI: Hawa ndio matajiri walio tajirika zaidi wakati wa Corona

Mabilionea Corona Hawa ndio matajiri walio tajirika zaidi wakati wa Corona

Mon, 17 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Janga la Covid -19 limefanya watu tajiri duniani kuendelea kuwa matajiri lakini limesababisha watu wengi kuishi katika umaskini, kulingana na shirika la misaada la Oxfam.

Watu wenye mapato ya chini zaidi duniani walichangia vifo 21,000 kila siku, ripoti yake inadai.

Lakini watu 10 tajiri zaidi duniani wameongeza maradufu utajiri wao wa pamoja tangu Machi 2020, Oxfam ilisema.

Oxfam kwa kawaida hutoa ripoti kuhusu ukosefu wa usawa duniani mwanzoni mwa mkutano wa Kiuchumi Duniani huko Davos.

Kongamano hilo kwa kawaida hushuhudia maelfu ya viongozi wa makampuni na kisiasa, watu mashuhuri, wanakampeni, wanauchumi na waandishi wa habari wakikusanyika katika eneo la mapumziko la Uswizi kwa ajili ya mijadala ya jopo, karamu za vinywaji na ushawishi.

Hatahivyo kwa mwaka wa pili mfululizo, mkutano huo (uliopangwa wiki hii)utafanyika mtandaoni baada ya kuzuka kwa aina mya ya corona ya Omicron ambayo imeathiri mipango ya kufanyika kwa mkutano wa watu kuhudhuria ana kwa ana.

Danny Sriskandarajah, mtendaji mkuu wa Oxfam GB, alisema shirika hilo la misaada linatoa ripoti yake ya kila mwaka sanjari na kongamano la Davos ili kuvutia umakini wa wasomi wa kiuchumi, biashara na kisiasa.

"Mwaka huu, kinachotokea ni nje ya kiwango," alisema. "Kumekuwa na bilionea mpya aliyeundwa karibu kila siku wakati wa janga hili, wakati asilimia 99 ya idadi ya watu duniani wanakabiliwa na hali mbaya zaidi kwa sababu yamasharti yaliyowekwa kudhibiti maambukizi ya virusi, biashara ya chini ya kimataifa, utalii mdogo wa kimataifa, na kutokana na hilo, watu milioni 160 zaidi wamesukumwa katika umaskini."

Kulingana na takwimu za Forbes zilizotajwa na shirika hilo la maaada, watu 10 tajiri zaidi duniani ni: Elon Musk, Jeff Bezos, Bernard Arnault na familia, Bill Gates, Larry Ellison, Larry Page, Sergey Brin, Mark Zuckerberg, Steve Ballmer na Warren Buffet.

Ingawa kwa pamoja utajiri wao ulikua kutoka dola bilioni 700 hadi dola trilioni 1.5, kuna tofauti kubwa kati yao, huku utajiri wa Bw Musk ukiongezeka kwa zaidi ya asilimia 1,000%, utajiri wa Bw Gates' uliongezeka kwa wastani wa asilimia 30.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live