Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

REA yafanikisha mradi wa umeme Iringa vijijini

Mgao Umeme.jpeg REA yafanikisha mradi wa umeme Iringa vijijini

Sun, 24 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi waTeknolojia za Nishati Jadidifu na Nishati Mbadala, Wakala wa Nishati Vijijini – REA, Mhandisi Advera Mwijage umesema atahakikisha washirikiana na Sekta binafsi katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora na nishati ya uhakika vijijini.

Mhandisi Mwijage ameyasema hayo baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa umeme wa maji (kilovoti 2400), wa Idete Wilayani Kilolo unaotekelezwa na Kampuni ya Lung’ali Natural Resources Co ltd.

Amesema, hadi kufikia sasa REA mpaka imetoa ruzuku ya Shilingi 4 Bilioni kwa mradi huo ulio chini ya Kanisa Katoliki Mkoa wa Iringa, ambazo zimetumika kwa utafiti wa mazingira, ujenzi wa Bomba la Maji na Jengo lenye mtambo wa kuzalishia umeme, (Power House).

“REA inafanya kazi na sekta binafsi ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora ya Nishati Vijijini na kuchangia katika shughuli za uchumi zinazoongeza kipato kwa Wananchi. Serikali haiwezi kufanya kila kitu katika miradi ya maendeleo inayogusa wananchi.” alisema Mhandisi Mwijage.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live