Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

REA kuanza kuwezesha ujenzi vituo vya mafuta nchini

UMEME Vunjwa REA kuanza kuwezesha ujenzi vituo vya mafuta nchini

Mon, 21 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetenga jumla y ash. Bilioni 12 kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa vituo vya mafuta maeneo ya vijijini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Dodoma kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wakala huo na mwelekeo wa Utekelezaji wa mwaka wa fedha 2023/24.

Amesema kuwa serikali imefikia uamuzi huo ili kuwawezesha wananchi wa vijijini wanapata nishati hiyo kwa bei rahisi zaidi tofauti na sasa ambapo wananunua kwenye chupa ambayo yanauzwa bei juu zaidi.

Mhandisi Saidy pia amesema kuwa ujenzi huo wa mafuta utapunguza madhara yanayoweza kutokea kutokana na wananchi kununua mafuta na kuyatunza ndani wanapoishi hali inayoweza sababisha mlipuko na maafa.

Amesema kuwa REA itakuwa ikiwezesha kupatikana kwa mkopo wa kuanzia shilingi Milioni 50 hadi 75 wenye riba ya asilimia 5 kwa muwekezaji mwenye lengo la kufanya uwekezaji huo kwa maeneo ya vijijini yasiyo na kituo cha mafuta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live