Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC atoa siku saba halmashauri kutathimini mfumuko wa bei

Bei Za Bidhaa 4.crdownload RC atoa siku saba halmashauri kutathimini mfumuko wa bei

Sat, 23 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ametoa siku saba kwa Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Wakuu wa wilaya kufanya tathimini ya kupanda kiholela kwa bei za bidhaa katika maduka na masoko mkoani humo.

Homera amesema leo Jumamosi Aprili 23,2022 wakati akizungumza na Mwananchi juu ya utekelezaji wa Agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alilolitoa jana kwa wakuu wa mikoa kufuatilia bei za bidhaa na kudhibiti mfumuko wa bei.

''Nimetoa siku saba kwa wakuu wa wilaya wakurugenzi wa halmashauri kuanza ufuatiliaji katika masoko na maduka ya wafanyabishara, wazalishaji kujiridhisha ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wafanyabishara.

''Pia wakati wa ufuatiliaji wafanyabishara washirikishwe katika kila maeneo lengo ni kutekeleza agizo la Waziri Mkuu na kudhibiti hali ya mfumuko wa bidhaa ambao umekuwa ukiumiza wananchi wa chini'' amesema

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Dk Vincent Anney amesema agizo hilo wamelipata jana na tayari utekelezaji wake umeanza kwa kuzunguka katika maeneo ya masoko na kuzungumza na wafanyabishara

''Kwa Rungwe tayari utekelezaji tumeanza tangu jana Mkuu wa Mkoa alipotoa  maelekezo na kwa imani kuanzia Jumatatu  zoezi litaendelea vizuri pia tunatoa elimu kwa wazalishaji wasitumie  fursa ya kupanda kwa bei ya mafuta kupandisha bidhaa''amesema.

Advertisement Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk Rashid Chuachua amesema kuwa utekelezaji wa agizo hilo utaanza rasmi Jumatatu Aprili 25 kwa kuzunguka maeneo mbalimbali ya jiji la Mbeya kujiridhisha hali halisi ya bei za bidhaa katika masoko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live