Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC akaribisha wawekezaji viwanda vya korosho

Ad1039448e41eaaada210f1714188b82 RC akaribisha wawekezaji viwanda vya korosho

Sat, 9 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa (RC) wa Ruvuma, Christina Mndeme, amewaita wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kwende kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa za kuongeza thamani katika zao la korosho.

Mndeme alitoa rai hiyo alipotembelea Kituo cha Utafiti wa Kilimo (Tari)- Naliendele kilichopo mkoani Mtwara ili kujionea kazi za utafiti mbalimbali zinazofanywa na kituo hicho ukiwemo utafiti wa kuongeza thamani katika mazao ya korosho, ufuta na karanga.

“Nitumie fursa hii kuwaalika wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili waje wajenge viwanda ndani ya Mkoa wa Ruvuma vya kuongeza thamani kwenye zao la korosho, zao la ufuta na karanga,” alisema.

Mdeme aliseme kazi kubwa ya utafiti imefanywa na Tari-Naliendele na sasa ni wakati sahihi wa wawekezaji kwenda kuwekeza katika mkoani humo.

Alisema Mkoa wa Ruvuma una maeneo ya kutosha, malighafi, nguvukazi, masoko, miundombinu ya barabara na umeme wa uhakika wa uhakika.

Kwa mujibu wa Mndeme, mwekezaji atakayewekeza katika Mkoa wa Ruvuma hatakutana na urasimu wowote na ndani ya wiki mbili, atapewa ardhi yake na hati Kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda kitakachoongeza thamani ya zao la korosho.

Alisema utafiti umefanya na unaendelea kufanya katika kuongeza thamani na pia, teknolojia ya kuzalisha bidhaa na kuongeza thamani ili nchi ijenge viwanda vitakavyozalisha bidhaa kama mvinyo wa korosho, juisi, siagi na maziwa.

Kaimu Mkurungezi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Naliendele, Dk Fortunatus Kapinga, alisema tekhnolojia ya kuzalisha bidhaa ipo kinachohitaji ni viwanda kwa ajili ya kuzalisha bidhaa za kuongeza thamani katika zao hilo.

Alisema kituo hicho ambacho kwa sasa kinazalisha bidhaa mbalimbali zikiwemo za mvinyo wa korosho, juisi na siagi kimefanya utafiti wa mazao ya kuongeza thamani na namna bora ya kuzalisha bidhaa hizo kupitua tekhnolojia.

Alisema ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani ya zao la korosho utapanga wigo wa soko, kuongeza uzalishaji na kuongeza ajira kwa wananchi huku ukimsaidia mkulima kuongeza kipato kutokana na mazao ya thamani ambayo awali yalitupwa kama taka.

Chanzo: habarileo.co.tz