Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC ahimiza uanzishwaji wa EPZA mji mdogo Mirerani

A8d504179dc3678b2f1ffaab6bf09795 RC ahimiza uanzishwaji wa EPZA mji mdogo Mirerani

Wed, 19 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Manyara, Joseph Mkirikiti amesema ipo haja ya kuhakikisha Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Mauzo ya Nje (EPZA) ya Mji Mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro inaanzishwa kwa lengo la kukuza uchumi wa mji huo.

Mkirikiti aliyasema hayo mjini Babati jana wakati akizungumza na viongozi wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Manyara (Marema) juu ya mikakati ya kuanzisha EPZA hiyo.

Alisema mpango wa EPZA Mirerani kujengwa kwenye eneo hilo ana taarifa yake na unapaswa kupewa kipaumbele upya.

"Rais John Magufuli amejinasibu kuwa yeye anaongoza Tanzania ya viwanda, hivyo EPZA Mirerani inatakiwa kuwekewa msukumo ili ifanye kazi katika eneo hilo,"alisema.

Alisema atahakikisha na yeye anafuatilia suala hilo ili kubaini mahali palipokwama kunusuru hali hiyo na kufanikisha utekelezaji wake kwenye ujenzi wake.

Mwenyekiti wa Marema, Justin Nyari alimshukuru Mkirikiti kwa kuliona hilo kwani kwa kiasi kikubwa uchumi wa eneo hilo utazidi kunyanyuka.

Nyari alisema EPZA Mirerani iliwekewa malengo kwa muda mrefu katika miaka iliyopita ila utekelezaji wake haukufanyika hadi hivi sasa.

Makamu Mwenyekiti wa Marema, Money Yusuf alisema serikali ilitenga eneo kubwa la ujenzi wa EPZA Mirerani lakini halijaendelezwa hadi sasa hivyo huu ni wakati mwafaka wa kutekeleza hilo.

Alisema endapo serikali itafanikisha hilo itakuwa inachochea uchumi kwa wananchi wa eneo hilo na majirani wanaozunguka mji mdogo wa Mirerani.

Chanzo: habarileo.co.tz