Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amesema uwekezaji wa Bandari ya Dar es salaam utasaidia kuinua kipato cha Wananchi wa Mkoa huo ambao wanategemea kilimo cha Alizeti na mazao mengine ya kibiashara.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amesema uwekezaji wa Bandari ya Dar es salaam utasaidia kuinua kipato cha Wananchi wa Mkoa huo ambao wanategemea kilimo cha Alizeti na mazao mengine ya kibiashara. Akiongea wakati wa Mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongollo Mkoani Singida, Serukamba amesema Wawekezaji wataongezeka kwani hakutakuwa na ucheleweshaji wa bidhaa zao kwenda nje ya Nchi na kutoharibika kabla hazijasafiri.