Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Songwe awataka wafanyabiashara kutoa ushirikiano TRA

IMG 20220621 WA0224 Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omari Mgumba

Tue, 21 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omari Mgumba amekutana na Maafisa wa Mamlaka wa Mapato TRA na kuishukuru Mamlaka hiyo kwa kuwatembelea walipakodi hao wa Mkoa wa songwe kwa ajili ya kutoa elimu mlango kwa mlango kufanya hivyo itapelekea uelewa mpana kwa wafanyabiashara wa Songwe kujua wajibu wa mamlaka na wajibu wakulipakodi.

Pia Mkuu wa mkoa aliendelea kwa kusema wafanyabiashara hao kutoa ushirikiano wa dhati kwa ajili ya kupata elimu ya kodi, kwakuhakikisha wasanimamia maneno na maelekezo ya Serikali ya Mh. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan bila kutumia nguvu, bila kutumia mabavu na bila kutumia hila, Mamlaka ya Mapato imekua ikikusanya kodi kwa weledi kukutana na wafanyabiashara kuwapa elimu ili kujua umuhimu wa kodi na madhara ya ukwepaji kodi.

Vilevile alitoa rai kwa wafanyabiashara wanapouza bidhaa watoe risiti na mnunuzi kudai risiti kwa kutokufanya hivyo ni kuikosesha mamlaka na serikali mapato yake halali na kudhoofisha juhudi za serikali.

Kwa upande wa Meneja wa Songwe wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Dickson Kimaro aliongezeza kwa kusema, ujio wa Maafisa hao kutoka Makao makuu utasaidia ongezeko la ukusanyaji wa mapato na kuondoa changamoto walizokuwa nazo walipakodi katika mkoa huo wa Songwe.

Naye Afisa uhusiano Mkuu Bw. MacDonald Mwakasindile kutoka Makao Makuu TRA amesema kuwa kuwa zoezi hili linafahamika kwa jina la mlango kwa mlango linalenga kuwahudumia wafanyabiashara ili kuangalia jinsi wanavyolipa kodi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live