Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mtwara haridhishwi na kasi ya malipo kwa wakulima wa korosho

34011 Pic+korosho Tanzania Web Photo

Sat, 29 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtwara. Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema haridhishwi na kasi ya ulipaji wa fedha za korosho kwa wakulima wa mkoa huo kutokana na kasi ya uhakiki ingawa alikiri kuwa nia ya Serikali ni njema na wakulima wote watalipwa.

Akijibu swali la mbunge wa Ndanda (Chadema) jana Ijumaa Desemba 28, 208 katika kikao cha kamati ya ushauri cha mkoa (RCC), Byakanwa alisema hadi kufikia Desemba 18 wakulima 104, 489 wamelipwa kiasi cha Sh106.8 bilioni.

Mwambe aliitaka Serikali kutoa tamko la kupokelewa kwa wanafunzi wote shuleni kuanzia Januari hata kama hawatakuwa na sare kutokana na baadhi ya wakulima kutolipwa fedha zao kama Serikali ilivyotangaza kununua korosho za wakulima.

“Mimi binafsi sikubaliani na kasi ya uhakiki tunayoenda nayo na malipo na mimi ningependa malipo yafanyike haraka iwezekanavyo, kama tutajiridhisha tutafanya kazi ya uhakiki kwa haraka na kama tutapata ushirikiano kwa wale ambao wanahakikiwa kuhakikisha kazi inafanyika mapema,” alisema Byakanwa

Alisema hata yeye katika vikao vya tathimini ameona kasi ya malipo ni ndogo ikilinganishwa na wakulima wanaozalisha lakini wanahitaji kwenda kujiridhisha na kuhakikisha wanamlipa mkulima mwenye jasho lake.

“Si kwamba dhana ya mwenye kilo zaidi ya 1,500 ndio anaweza kuwa amelangua korosho, ilitumika ili kuonyesha tuanze malipo kuliko kuanza kuhakiki watu wote ndipo tuanze malipo, nadhani kilio kingekuwa kikubwa zaidi,” alisema Byakanwa

Alisema sasa kama mkoa wanataka wafikie kiwango cha kulipa Sh20 bilioni kila siku kutoka Sh12 bilioni lakini bado wanaishauri na kushirikiana na Wizara ya Kilimo kuhakikisha kasi ya malipo inaongezeka ili kutumia muda mfupi kuwalipa wakulima.

“Taarifa ambazo ofisi yangu inazo, tuna wakulima zaidi ya 2,800 ambao pesa zao zimegoma kulipwa benki kwa sababu tofauti tofauti.”

“Mosi majina aliyotuambia mkulima ni tofauti na akaunti, lakini wakulima wengine walipouza korosho msimu uliopita waliondoa fedha zote sasa anapoileta akaunti alipwe iko domant,” alisema Byakanwa.

 

Awali Mwambe alisema wanunuaji wa kangomba hawazidi asilimia 20 lakini kasi ya malipo haiendani na waliohakikiwa licha ya kuwa wakulima wanahitaji fedha.



Chanzo: mwananchi.co.tz