Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Makalla alitaka Jukwaa la Wanawake kuleta mabadiliko ya kiuchumi

MAKALLA 1 RC Makalla alitaka Jukwaa la Wanawake kuleta mabadiliko ya kiuchumi

Wed, 3 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ameelekeza Jukwaa la uwekezaji Wanawake kiuchumi Mkoa huo kuja na mpangokazi wa kuleta mabadiliko chanya kwa Wanawake ikiwa ni pamoja na kuwafikia wengi zaidi Ili kuleta tija na mabadiliko ya kiuchumi.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati ufunguzi wa Mafunzo maalumu kwa Viongozi wa majukwaa ya Wanawake Mkoani humo ambapo ameelekeza mafunzo waliyopata wakayashushe ngazi ya Wilaya, Kata na mitaa Ili kunufaisha Wanawake wengi zaidi.

Aidha, Makalla ameelekeza dhana ya uwezeshaji Wanawake kiuchumi iende sambamba na kuwapatia fursa mbalimbali zinazopatikana Ili kuwakwamua kiuchumi.

Pamoja na hayo RC Makalla amesema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan alilotoa kwa Kila Mkoa kuyalea na kuyatunza Majukwaa ya Wanawake.

Sanjari na hayo, Makalla amewataka Viongozi wa majukwaa ya Wanawake kuelimisha Wanawake Kuhusu umuhimu wa kufanya mambo machache kwa ufanisi na tija na sio kujaribu Kila biashara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live