Mkuu wa Mkoa wa Pwani Aboubakar Kunenge amesema hatokubali Taasisi yoyote ya Serikali kuja kuwa kikwazo kwa Wawekezaji wanaojenga Viwanda vya SINOTAN Kibaha Mkoani Pwani.
RC Kunenge ametembelea eneo la uwekezaji kongani ya viwanda SINOTAN kibaha Pwani leo na kukutana na Mwekezaji wa SINOTAN ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Jansen Huang na kusema yafuatayo.
“Sitokubali wakati Wawekezaji wameshaanza kujenga wanaendelea ndio Taasisi ya Serikali inakuja na kuwa kikwazo kwa Wawekezaji, Taasisi yoyote ya Serikali isiwe kikwazo sitokubali Taasisi za kisekta, Wizara za kisekta au za Halmashauri kuwa kikwazo kuturudisha nyuma" ——— amesema RC Kunenge.