Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Chalamila awatoa hofu wafanyabiashara Kariakoo

Albert Chalamila RR RC Chalamila awatoa hofu wafanyabiashara Kariakoo

Sun, 25 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati soko la Karikaoo likitarajiwa kumalizika ujenzi wake Oktoba mwaka huu, Serikali inatarajia kuingia mkataba na wafanyabiashara wote watakaorejea sokoni hapo.

Wakati soko la Karikaoo likitarajiwa kumalizika ujenzi wake Oktoba mwaka huu, Serikali inatarajia kuingia mkataba na wafanyabiashara wote watakaorejea sokoni hapo. Hayo yamesemwa leo Juni 24, 2023 na Mkuu wa Mkoa huo, Albert Chalamila, alipotembelea kuona maendeleoo ya ujenzi wake. Chalamila alisema sambamba na kuingizwa kwa mkataba, pia wafanyabiashara wataliazimika kulipa kodi ya kawaida itakayokuwa imepangwa kwa kuwa gharama ya Sh28 bilioni zilizoingizwa katika ujenzi na ukarabati wa soko hilo na Rais Samia Suluhu Hassan, zitatakiwa zirudi. “Huu ni mkopo kwenu kwa wenzetu nyie wa Kariakoo hivyo lazima mjiendeshe kwa kukusanya fedha hizo na kuzirejesha ili ziweze kujenga majengo mengine kama haya maeneo memgine.”amesema Chalamila. Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa mkoa aliwatoa hofu wafanyabishara waliokuwa sokoni hapo kuwa mpaka sasa hakuna chumba hata kimoja ambacho tayari kimeshagawiwa sokoni hapo na kueleza kuwa shughuli hiyo itakapoanza utaratibu wa kugawa utakuwa wazi. Hata hivyo alipongeza maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa soko hilo na kueleza kuwa ameridhishwa pia na kasi pamoja na viwango vyake. Amesema kukamilika kwa soko hilo, amesema kutasaidia katika kufanya biashara shindani zitakazofanyika kwa saa 24 na kinachofanyika sasa katika katika kuelekea huko ni kuweka taa na CCTV camera katika viunga mbalimbali vya Karikaoo ili kuimarisha usalama nyakati zote za ufanyaji biashara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live