Kampuni ya simu ya Oppo pamoja na Samsung wamesema kuondolewa kwa Kodi (VAT) kwenye simu janja kutaongeza wigo wa matumizi ya simu hizo kwa watanzania.
Bunge la Bajeti la mwaka 2021/22 limeondoa kodi ya asilimia 18 kwenye simu janja ili kila mwananchi aweze kutumia simu hizo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mkuu wa Usambazaji wa Bidhaa za kampuni ya Oppo Mbwana Mtopa amesema serikali imefanya jambo kubwa sana kwa kuondoa kodi katika simu janja ili ili kila mtanzania aweze kumiliki.
Amesema, wao kama kampuni ya Oppo wamejipanga kuweza kuhakikisha simu zao zinakuwa katika bei nzuri na kila mwananchi anapata fursa ya kumiliki simu janja na kuwa katika ulimwengu wa Kidigitali.
“Dunia imekuja ni kijiji, leo Oppo na Samsung tumezindua kwa pamoja duka hili katika jengo la China Plaza ukifika utapata simu aina zote na kwa beo nzuri lakini kikubwa ni kuondolewa kwa VAT hii inapelekea kwa sisi makampuni kupunguza bei za simu janja ili wananchi hadi wa kipato cha chini waweze kumiliki,”amesema
Naye Kwa upande wa Meneja bidhaa kutoka Samsung Julius Giabe amesema kwa sasa kuna soko kubwa la ushindani ukizingatia makampuni ya simu ni mengi ila kwa upande wao wamejipanga kuleta bidhaa zenye ubora na uwezo mkubwa.
Giabe ameishukuru serikali kwa kuondoa kodi (VAT) kwa simu janja na hiyo ni chachu ya kufanikisha Tanzania katika dunia ya kidigitali.
Oppo na Samsung wamezindua duka la pamoja litakalokuwa linauza bidhaa zake ili kuwafikia wateja wao kwa urahisi zaidi na kuishukuru serikali kwa kuondoa kodi (VAT) kwa simu janja (smartphone).
Duka hilo limezinduliwa leo na kuwataka wateja wa kampuni hizo kufika na kujionea ubora wa simu zao.