Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Qatar yakaribishwa kuwekeza Tanzania

WhatsApp Image 2022 10 05 At 11.34.30 AM.jpeg Qatar yakaribishwa kuwekeza Tanzania

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: EATV

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Qatar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Ukarimu wa Katara Mhe. Ali bin Ahmed Al Kuwari na ujumbe wake, Doha nchini Qatar.

Katika mkutano huo, wamezungumzia masuala ya kikodi baina ya Tanzania na Qatar, uwekezaji, biashara, sekta ya nishati ya gesi, ufugaji, utalii pamoja na Kilimo.

Kuhusu uzoefu kwenye masuala ya utalii nchi ya Qatar wamepiga hatua kubwa kwenye sekta hiyo hususan ukarimu kwa wageni, pamoja na jinsi ya uendelezaji wa miundo mbinu.

Katika suala la afya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pia amekutana na kuzungumza na Waziri wa Afya wa Qatar Dkt. Hanan Mohamed Al Kuwari ambapo wamejadiliana mambo mbalimbali yatakayonufaisha Tanzania katika sekta ya Afya.

Huku wakikubaliana kubadilishana wataalamu kuongeza uzoefu kwenye sekta hiyo ya afya ambapo Qatar kwasasa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika utoaji wa huduma na vifaa vya kisasa.

Hata hivyo Waziri wa Afya wa Qatar amesema wapo tayari kutoa mafunzo kwa wataalamu wa Kitanzania katika sekta hiyo ya afya hasa katika huduma za dharura pamoja na za kibingwa

 

Chanzo: EATV