Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pwani wapongezea bajeti ya kilimo

B663b9a8895cb2b1ff0d5678bc69952c Pwani wapongezea bajeti ya kilimo

Sat, 21 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkoa wa Pwani umeipongeza serikali kwa kuitengea Wizara ya Kilimo, bajeti kubwa ili kupunguza changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Sara Msafiri ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani, wakati wa maadhimisho ya siku ya Mkulima yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Kibaha.

Jumatano wiki hii, Bunge lliidhinisha jumla ya Sh 751,123,280,000 kwa ajili ya bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka 2022/ 2023, ikiongezeka kutoka Sh. 294,162,071,000 za mwaka uliopita, sawa na ongezeko la asilimia 155.34.

Msafiri amesema bajeti hiyo haijawahi kutokea, ambapo imeonesha jinsi gani serikali ilivyotoa kipaumbele kwenye sekta ya kilimo, ili ilete mapinduzi.

Amesema kilimo ni kila kitu, endapo kila mhusika atatumia ujuzi na maarifa yake, ambapo serikali kwa upande wake tayari imeshawezesha kwa masuala ya bajeti na wataalamu kwa kuwapatia vitendea kazi.

Naye Meneja wa TARI Kibaha, Hildelitha Msita, amesema kuwa maadhimisho hayo yamefanyika kituo hicho kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali wakulima kutoka kwenye baadhi ya halmashauri za mkoa huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live