Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pura yaja na mwarobaini kupata wafanyakazi mahiri

Gesiii Pura yaja na mwarobaini kupata wafanyakazi mahiri

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ili kupata waajiriwa wenye sifa na wataalamu wabobezi, Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (Pura) imeanzisha mfumo wa kuwasajili watoa huduma katika sekta ya mafuta na gesi asilia.

Mfumo huo wa kidigitali unaojulikana kwa jina la ‘Common Qualification System’ (CQS) utakaokuwa na makundi matatu, utawezesha kutambua wanaotaka ajira na lakini pia kukusanya taarifa kwa njia ya mtandao ili kubaini fursa na changamoto.

Mkuu wa Kitengo cha Maudhui ya Ndani na Mshirikishaji wa Wadau kutoka (Pura) Charles Nyangi alisema, baada ya mfumo huo kuanza kazi watapaswa kujisajili na kuutumia kuwasilisha taarifa zao moja kwa moja.

Sababu nyingine ni pamoja na kuangalia wataalamu, maudhui ya ndani ya kampuni husika pamoja na uwezo wa watoa huduma.

“Mfumo huu unaweza kujua uwezo wa mtu, idadi ya wataalamu na kiwango cha elimu kwa watu wanaofanya kazi kwenye sekta hiyo ya mafuta na gesi,”alisema.

“Malalamiko mengi yamekuwa yakitolewa kwa kampuni nyingi ikiwemo za ulinzi na usafi, kufanya hivi kama Serikali ni kujua uwezo wetu na wa kampuni zetu,”alisema Nyangi.

Nyangi alisema dhumuni lingine la kuanzisha mfumo huo ni kama kampuni haiandai taarifa zake za mwaka au kuhusisha leseni zao na kuwasaidia kazi wanazofanya kuangalia kama zinatekelezeka.

“Shughuli ya utafutaji wa mafuta na gesi ilikuwa imeshuka kadri tunavyokwenda inaongezeka, zinavyoongezeka watoa huduma watatumia mfumo huu kutafuta vitu mbalimbali ikiwemo ajira,”alisema.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Aly Mluge alisema mafunzo hayo yanahusisha mfumo wa kupata taarifa za wazawa katika shughuli mbalimbali za mafuta na gesi kwa mkondo wa juu.

Alisema awali walikuwa wakitumia sana mfumo wa karatasi kuwasilisha taarifa husika, kuanza kwa mfumo huo wataanza kutumia njia ya mtandao itakayowarahisishia majukumu yao na kuokoa muda.

“Kama mnavyojua dunia imepiga hatua tuwapongeze Pura na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) kwa namna wanavyowezesha wadau namna ya kuwasilisha hizi taarifa,”alisema Mluge.

Julai mwaka huu Mamlaka hiyo ilieleza kuwa miradi itakayotekelezwa kupitia uwajibaki kwa jamii (Corporate Social Responsibility - CSR), itakuwa ni yenye kuakisi mahitaji ya yatokanayo na vipaumbele vya jamii husika.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Pura, Charles Sangweni, katika kikao cha uwasilishaji wa rasimu ya mwongozo wa CSR wa kampuni zitakayotekeleza miradi hiyo kwa jamii, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Julai 19, 2023.

"Huu mwongozo utasaidia, pamoja na mambo mengine, kuhakikisha kuwa miradi ya CSR inayotekelezwa na kampuni zinazofanya shughuli za utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini ina akisi mahitaji ya jamii hizo kulingana na vipaumbele vya jamii husika," alisema bosi huyo hivi karibuni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live