Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Punguzo la kodi vitenge kukuza uchumi

Vitenge  Maroboita Punguzo la kodi vitenge kukuza uchumi

Tue, 15 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya mapato nchini (TRA) imesema kuwa kupunguzwa kwa kodi ya thamani ya uingizaji vitenge kutoka nje ya nchi kutaondoa changamoto ya wafanyabiashara kukimbia kupitisha bidhaa zao njia halali na kukimbilia kwenye njia za panya.

Meneja wa TRA mkoa Kigoma, Deogratius Shuma alisema hayo akizungumza katika semina ya siku moja kwa wafanyabiashara,wasafirishaji shehena na mawakala wa ushuru wa forodha mkoani ambapo alibainisha kwamba kodi hiyo itakuwa rafiki na wafanyabiashara watalipa kodi kwa halali.

Shuma amesema kuwa anaamini kwa hali hiyo kutawezesha mamlaka hiyo mkoa Kigoma kuongeza ukusanyaji wa mapato wa bidhaa zinazoingizwa kutoka nje lakini pia utawezesha kufikia lengo la ukusanyaji mapato wanalojiwekea.

Wakizungumzia kupunguzwa kwa kiwango hicho cha kodi Wafanyabiashara wa vitenge mkoani Kigoma wamesema kuwa punguzo la kodi ya ongezeko la thamani kwa ajili ya uingizaji wa vitenge nchini kutoka nje ya nchi kutawawezesha kufanya biashara zao vizuri na kuondokana na kufanya biashara hizo kwa njia zisizo halali (Njia za panya).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live