Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Programu ya kilimo viwanda kunoa wanafunzi

Viwanda Biashara.png Programu ya kilimo viwanda kunoa wanafunzi

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika jitihada za kuinua sekta ya kilimo nchini, Serengeti Breweries (SBL) imetangaza ufadhili kwa wanafunzi wanaojiunga na masomo ya Kilimo katika Shule ya St Maria Goretti ya mkoani Iringa.

Kampuni hiyo imesema safari hii inatoa ufadhili huo kwa wanafunzi wapya watano watakao jiunga na wenzao tisa wanaoendelea na masomo hayo shuleni hapo na kufanya idadi ifikie 14.

Hata hivyo, katika programu hiyo ya ufadhili, zaidi ya wanafunzi 300 wanaosoma kozi ya kilimo katika maeneo tofauti nchini, wamenufaika, huku walengwa wakiwa ni wanafunzi wanaotoka familia duni.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Obinna Anyalebechi amesema, “Ufadhili huu ni sehemu ya ahadi yetu ya kusaidia maendeleo ya kilimo nchini.”

Obinna anaamini kuwa programu hiyo itaimarisha rasilimali ya wataalamu wa kilimo nchini ambao pia watawasaidia wakulima kuongeza tija kwenye uzalishaji na hatimaye mapato.

Amesema, “Mwaka huu, tutawasaidia wanafunzi wapya watano ambao watajiunga na wanafunzi tisa ambao tayari wanasomea taaluma za kilimo katika Shule ya St Maria Goretti huko Iringa.”

Awali, Mkurugenzi wa Mnyororo wa Ugavi kutoka kampuni hiyo, Alfred Balkagira amesema programu hiyo inachochea vipaji vya ndani sambamba na kuongeza uwezo wa upatikanaji wa malighafi zinazozalishwa nchini.

“Hatua hii situ inapunguza gharama, bali pia inachangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa jamii za wakulima zinazozunguka, ikijenga uhusiano thabiti kati ya SBL na jamii ya eneo husika,” amesema Balkagira.

Amesema wanafunzi wanaosoma kupitia program hiyo wanatarajiwa kuwa mabingwa wa mbinu endelevu za kilimo, na hivyo kuathiri kwa njia chanya mchakato wa upatikanaji na uzalishaji.

“Dhana zao mpya na mawazo ya ubunifu zitasaidia kuongeza ufanisi na kusawazisha upatikanaji wa malighafi za SBL kutoka kwa wakulima kwa ajili ya uzalishaji wa bia, kama shayiri, mahindi na mtama,” amesema Balkagira.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live