Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Programu mafunzo fursa za utalii yaja

Prof Mahalu Programu mafunzo fursa za utalii yaja

Mon, 11 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

PROGRAMU ya mafunzo ya kuhusu namna bora ya kuendesha, kukuza na kutambua fursa zilizopo kwenye sekta ya utalii nchini inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni jijini Mwanza.

Alisema SAUT na RPR zinafanya kazi kwa mashauriano ya karibu na washirika wengine ili kusaidia sekta ya utalii na kuhakikisha sekta hiyo inarejea kikamilifu, huku pia wadau wakichukua tahadhari zote za kiafya dhidi ya virusi vya corona. Aliongeza kwamba mpango pia unalenga kuwaandaa vizuri wakazi wa Kanda ya Ziwa ili wawe mstari wa mbele kuunadi utalii uliopo kanda hiyo.

“Tunatarajia kwamba awamu ya kwanza ya programu yetu itaanza na Jiji la Mwanza ambapo tunalenga kuwafikia wadau wengi iwezekanavyo watakaotoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza ambapo tumejipanga kupokea watu wasiopungua 2000 watakaopata mafunzo kwa awamu, alisema, huku akiitaja mikoa itakayofuata kuwa itakuwa ni Geita, Simiyu, Shinyanga, Mara na Kagera.

Alisema katika utoaji wa mafunzo hayo umeandaliwa mpango kabambe utakaohakikisha washiriki wanajikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona ikiwamo kuendesha mafunzo hayo kwenye maeneo ya wazi ili kuepuka msongamano kwenye eneo dogo.

Naye Mkurugenzi wa Real PR Solutions Kanda ya Ziwa, Magreth Laizer, alisema kampuni hiyo imejipanga kuhakikisha inafanikisha ukusanyaji wa fedha kutoka kwa wadau mbalimbali hasa wa utalii kuwezesha uendeshaji wa programu hiyo muhimu.

Mbali na mikoa ya Kanda ya Ziwa, Laizer aliitaja mikoa mingine itakayoguswa ni Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Songwe, Njombe, Mtwara, Ruvuma, Lindi, Dodoma, Singida, Tanga, Manyara, Dar es Salaam, Morogoro na Pwani.

Aidha, katika kuuboresha zaidi ufanisi wake, mpango huo pia utahusisha kampuni ya PEAL Performance iliyojikita kwenye masuala ya uendelezaji ustadi wa watu hususani katika sekta ya utalii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live