Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa Muhongo ataja mambo matano kukuza uchumi

Muhongo Pic Data Profesa Muhongo ataja mambo matano kukuza uchumi

Tue, 9 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospiter Muhongo ametaja mambo matano ambayo yatasaidia Tanzania kwenda mbele kiuchumi.

Hata hivyo Profesa Muhongo amesema bila ya kufikia asilimia 10 ya ukuaji wa uchumi, Watanzania watambue kuwa bado wanaishi katika umasikini.

Mambo aliyotaja ni kwamba yanaweza kuipeleka Tanzania kwa haraka ni Kilimo, Elimu, Afya, Miundombinu, Mazingira na tabia nchi.

Waziri huyo wa zamani wa Nishati na Madini amesema uchumi wowote katika taifa kama utakuwa chini ya asilimia 10 katika ukuaji wake, watu hao watambue bado wako katika taifa masikini.

"Lakini hata katika Kilimo, lazima tuangalie mambo machache kuwa tulime mchele, ngano, mahindi na mihogo ambavyo ndivyo vinatakiwa kwa sasa duniani," amesema Muhongo.

Katika mchango wake Profesa, amerudia ushauri wake kuhusu Taifa kujiwekea akiba ya dhahabu kama ilivyo kwa mataifa mengine ambayo itasaidia pale uchumi unapoyumba.

Profesa Muhongo ni mtaalamu katika masuala ya madini na miamba amekuwa akizungumzia kuhusu uchimbaji madini ambayo baadhi anasema yasipochimbwa sasa kuna mataifa yameshaingia mkataba kuyachimba mwezini.

Kingine amezungumzia ujenzi wa barabara wa Kilomita chache kila maeneo kwamba siyo mpango mzuri wa kulisaidia Taifa.

Chanzo: mwananchidigital