Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa Mkenda: Tutawashughulikia watakaokwamisha uzalishaji sukari

9ab5bcb7682484fc502fb99fa25f11b0 Profesa Mkenda: Tutawashughulikia watakaokwamisha uzalishaji sukari

Thu, 18 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Serikali imesema kuna mbinu chafu za watu kukwamisha uanzishaji wa viwanda vipya vya sukari nchi ili kupuinguza uhaba wa serikali unaojitokeza mara kwa mara nchini.

Akizungumza na wakulima wa miwa katika bonde la Mbigiri Wilayani Kilosa, mkoani Morogoro, Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda amesema Serikali imegundua na imejipanga kukabiliana na njama hizo ili kuhakikisha viwanda vingi vinafunguliwa ili kuongeza ushindani katika soko la miwa kwa wakulima.

Profesa Mkenda amesema licha ya uzalishaji wa miwa kuwa mkubwa lakini Tanzania bado ina upungufu wa sukari na tatizo likitajwa ni uwezo wa viwanda vilivyopo kuwa na uwezo mdogo kuchakata miwa hiyo.

"Niwaombe wale wote wanaotaka kuanzisha viwanda vya sukari waje kufanya hivyo na serikali tutawalinda, na yeyote atakayekwamisha tutashughulika naye,” alisisitiza Profesa Mkenda.

Waziri Profesa Mkenda amemaliza ziara yake ya siku tatu ya kutembelea wakulima wa miwa na uongozi wa viwanda vya sukari mkoani Morogoro kuangalia namna bora ya kuendeleaza zao la miwa ili kupunguza nakisi ya sukari ya tani 40,000 ambayo Tanzania uagiza kutoka nje.

Chanzo: habarileo.co.tz