Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa Kitila ampongeza mwekezaji wa kiwanda Longido

Kitila Pc Data Waziri wa Viwanda, Prof Kitila Mkumbo

Mon, 18 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo amempongeza mwekezaji wa Ariya Foods Company Limited aliyejenga kiwanda cha kusindika nyama wilayani Longido mkoani Arusha, akisema kiwanda hicho ni miongoni mwa viwanda 618 vikubwa nchini.

Profesa Mkumbo ameyasema ameyasema hayo leo Oktoba 18 wilayani Longido, kabla Rais Samia Suluhu Hassan ahajazindua kiwanda hicho ambacho ni miongoni mwa viwanda vitano vikubwa mkoani humo.

Amesema hadi Julai 2021 kazi data ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inaonyesha kuwa Tanzania ina viwanda 80,969 vikiwemo viwanda 285 vilivyopo Arusha.

“Namshukuru mwekezaji Ariya Foods Company Limited huyu ambaye leo tumezindua kiwanda chake na kuongeza idadi ya viwanda ambayo mazao yake yanaifanya nchi kuwa na viwandda 10 vya kusindika nyama,” amesema na kuongeza:

“Eneo ambalo tumezindua kiwanda ni maeneo ya Ukanda Maalum wa Kiuchumi (EPZA). Ni miongoni mwa 160 tuliyonayo nchi nzima na kwa Arusha yapo tisa. Yanasaidia kuongeza idadi ya usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi na hivyo kutupatia fedha za kigeni,” amesema.

Chanzo: mwananchidigital