Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prof Ole Gabriel ataka uwekezaji sekta ya mifugo, mbegu za malisho

WhatsApp Image 2021 05 13 At 18.01.48.jpeg Prof Ole Gabriel ataka uwekezaji sekta ya mifugo, mbegu za malisho

Fri, 14 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Prof  Ole Gabriel, ametoa rai hiyo wakati akifungua warsha maalum ya wadau wa uzalishaji mbegu za malisho hapa nchini ili kijadili namna kuongeza uzalishaji wa mazao ya mifugo nchini na upatikanaji wa malisho bora kwa kipindi cha mwaka mzima

Amesema kuwa takwimu zinaonesha  kiwango cha uzalishaji wa mbegu ni mdogo ukilinganisha na mahitaji yake na kwamba kama wawekezai wakigeuza changamoto hiyo kuwa fulsa inasadia kwa kiasi kikubwa kuongeza uzalishaji

“Mahitaji ya mbegu za malisho nchini  ni tani milioni 7 lakini kiwango cha  mbegu kilichozalishwa kwa mwaka 2019/20 ni tani 127 maana yake ni kwamba kuna uhaba mkubwa sana ivyo changamoto hiyo tubadilishe kama fursa ya uwekezaji wa kibiashara ” amesema Prof Gabriel

Kadharika amesema serikali kupitia wizara ya mifugo na uvuvi itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo na makampuni na watu binafsi wenye nia ya kuzalisha mbegu bora za malisho, kufanya kazi hii kibiashara kwa kuwapa mwongozo unaostahili.

Amebainisha kuwa lengo ni kufanikisha juhudi hizi za serikali hasa kujiletea faida za kiuchumi kupitia uwepo wa fursa ya wingi wa mifugo nchini na hata kuuza malisho katika mataifa mengine

“Hii si tukwamba itainua uchumi wa mtu binafsi bali italipatatia taifa fedha za kigeni hasa tukizingatia kuwa wananchi wanaweza kutumia fursa ya ardhi iliyopo kuzalisha malisho kibiashara kama wanavyo zalisha mazao ya chakula”. amesema Prof Gabriel

Kwa upande wake Mkurugenzi idara ya utafiti mafunzo na huduma za ugani, Angelo Mwilawa amesema lengo la walsha hiyo ni kuhakikisha tafiti zilizofanyika kubaini mbegu bora za malisho zinawafikia wafugaji wadogo kwenye mashamba yao

Amesema zipo mbegu ambazo zimekuwa rahisi kuwafikia wafugaji kama mbegu aina ya nyasi, mikunde inayoa taambaa na mikunde ya miti ambazi zipo katika makundu tofauti ambazo pia mahitaji ya msingi katika mashamba ya malisho.

 “Tunaona kuna fulsa kubwa yauzalishaji wa  mbegu endelevu na hapa tunazungumza mbegu mafungu matatu ambazo hizo tunaangalia ni namna gani tunaongeza uzalishaji hapa nchini” amesema Mwilawa

Chanzo: ippmedia.com