Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo ameweka wazi sababu zinazochangia sekta ya madini kushindwa kuchangia vyema katika uchumi kuwa ni pamoja na kujishughulisha na utawala wa sekta ya madini 'administration of the mineral sector'.
Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo ameweka wazi sababu zinazochangia sekta ya madini kushindwa kuchangia vyema katika uchumi kuwa ni pamoja na kujishughulisha na utawala wa sekta ya madini 'administration of the mineral sector'. Amesema utaratibu huo umelifanya taifa kuweka nguvu katika uchimbaji wa madini ya aina moja - dhahabu, almasi na vito (Tanzanite na Rubi). "Wasinge shughulika na mambo ya utawala sana, chuma ya Liganga ingekuwa imeshachimbwa," amesema na kuongeza kuwa Uchumi unapaswa kukua kwa asilimia 8 hadi 10, kuondoa umasikini.