Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prof. Mkumbo Aongoza Kikao Cha 32 Cha Bodi ya Wakurugenzi Wa EPZ

2 12 Scaled?fit=2560%2C1707&ssl=1 Prof. Mkumbo Aongoza Kikao Cha 32 Cha Bodi ya Wakurugenzi Wa EPZ

Thu, 20 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Waziri wa Viwanda na Biashara na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa EPZA, Prof. Kitila Mkumbo akizungumza.

Waziri wa Viwanda na Biashara na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa EPZA, Prof. Kitila Mkumbo ameongoza kikao cha kawaida cha 32 cha bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya nje (Export Processing Zones Authorty -EPZA).

Kikao kimefanyika leo Mei 19, 2021 Jijini Dodoma katika ukumbi wa Mkutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Jengo la Mkapa na  kimeudhuliwa na viongozi mbalimbali; Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dotto James, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Mathew Mnali na wajumbe wengine wa bodi ya wakurugenzi wa EPZA.

Kikao hicho kimekuwa na lengo la kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ripoti ya Mkurugenzi wa EPZA kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2021, Makadirio ya mapato na matumizi ya Mamlaka ya (EPZA) kwa mwaka 2021/2022, utaratibu wa kuendeleza Mradi wa kurasini SEZ, mradi wa kubangua korosho kwa kushirikiana na wajasiriamali (SMEs) na mengineyo

Chanzo: globalpublishers.co.tz