Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yaonya wanaotorosha mifugo nje

71718971689e07e020e6d2871d6b2cae Polisi yaonya wanaotorosha mifugo nje

Mon, 6 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Kikosi Cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Tanzania (STPU), Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Simon Pasua ametangaza vita na watoroshaji wa mifugo nje ya nchi.

Amesema hayo leo, Juni 6, 2022 wakati akizungumza na askari wa kikosi hicho wa Makao Makuu Jijini Arusha na kueleza kuwa zipo taarifa za watu wachache wanaojihusisha na utoroshaji wa mifugo nje ya nchi na kuonya kikosi chake hakitakuwa na huruma na wanaojishughulisha na jambo hilo.

Amewataka watendaji wa kikosi hicho wasijihuishe kwa namna yoyote na watuhumiwa wenye lengo la kutorosha mifugo.

Pia amewataka wafugaji kote nchini kufuata taratibu za uuzaji wa mifugo yao, ili kuongeza patao lao na taifa kwa ujumla.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live