Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Poland kuisaidia Tanzania kuimarisha mfumo wa kodi

Mwigulu Nchemba Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Sat, 21 Jan 2023 Chanzo: eatv.tv

Poland imeahidi kuisadia Tanzania kuimarisha mifumo ya kodi kwa njia ya kidigitali ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa ajili ya kuendeleza nchi na watu wake kwa ujumla.

Ahadi hiyo imetolewa Mjini Davos nchini Uswisi na Waziri wa Fedha wa nchi hiyo, Mheshimiwa Magdalena Rzeczkowsk, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Amesema kuwa mpango huo utatekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja ambapo Poland itatumia uzoefu wake katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa njia ya kielektroniki kuifanya Tanzania pia iwe na uwezo huo ili kuimarisha ukusanyaji wa mapato yake ya ndani kwa njia ya kodi

Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameishukuru Poland kwa uamuzi wake wa kuisaidia Tanzania katika suala hilo la kuwezesha ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya serikali kidigitali pamoja na kuahidi kuisadia Tanzania katika kutekeleza miradi ya kiuchumi katika nyanja mbalimbali kikiwemo kilimo.

Aidha, Akizungumzia kuhusu mkutano wa 53 wa Jukwaa la Uchumi Duniani lililofanyika Davos, nchini Uswisi, ambapo Tanzania iliongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Nchemba alisema kuwa mkutano huo umekuwa na mafanikio makubwa kwani umeiwezesha Tanzania kunadi sera zake za kiuchumi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Chanzo: eatv.tv