Dar es Salaam. Pizza Hut Tanzania, imemaliza mwaka 2019 kwa kishindo,kwa kufungua mgahawa wa nane nchini uliopo katika jengo la Mikocheni Plaza, ambao ulifunguliwa rasmi katika mkesha wa mwaka mpya ikiwa ni wa pili kufunguliwa katika mwezi huo ambapo pia imefungua mgawaha mpya wenye viwago vya kimataifa katika uwanja mpya wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere International Airport (JNIA), Desemba 16, 2019.
Migahawa mingine ya Pizza Hut ipo katika maeneo ya Mlimani City, Oysterbay Mall, Mkuki House, Shoppers Plaza, Peugeot House na mjini Arusha katika eneo la maduka ya TFA .
Kampuni ya Dough Works Ltd, ambayo inamiliki mtandao wa migahawa hiyo imesema inafurahi kufungua mgahawa wa nane nchini Tanzania na pia inajivunia kupitia uwekezaji huo kuweza kuzalisha ajira zaidi ya 400.
“Tunayo furaha kuona biashara yetu inazidi kukua na kuwafikia wananchi wengi na bidhaa zetu za Pizza, zenye viwango vya kimataifa kuzidi kufurahiwa na wateja wetu”. alisema Vikram Desai, Mkurugenzi Mkuu katika hafla ya uzinduzi wa mgahawa mpya wa Pizza Hut wa Mikocheni Plaza iliohudhuriwa na wadau mbalimbali ikiwemo wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Mbali na kusherekea kufungua migahawa mipya ya Pizza Hut, Kampuni ya Dough Works Ltd, kwa sasa inaendesha mtandao wa migahawa 4 ya KFC kuanzia Oktoba 3, 2019.
“Katika kipindi cha miezi 3 mtandao wa migahawa ya KFC imeongeza migahawa 6 baada ya kufunguliwa migahawa mipya miwili mwezi Desemba mwaka jana.Kwa sasa migahawa ya KFC iko katika maeneo ya Kariakoo, Diamond Plaza,Mlimani City,Uwanja wa ndege mpya wa JNIA na Mikocheni Plaza, Kampuni inayo mpango wa kupanua huduma zake zaidi kufikia maeneo mengine ili ziwafikie wananchi wengi zaidi,” alisema Mkurugenzi wa Dough Works Ltd,Vikram Desai.
Pia Soma
- Homa ya tamasha la Sauti za Busara yazidi kupanda Zanzibar
- Marekani yampongeza Magufuli, yasisitiza tume huru ya uchaguzi
- Lugola ahojiwa na Takukuru kwa saa tano
Mtandao huo kwa sasa una migahawa 14 ya KFC na Pizza Hut, ambayo inahudumia zaidi ya watu 1,000 ambao hufika kupata chakula na pia inatoa huduma za kusambaza chakula chake maarufu cha Pizza na kuku maofisini mpaka majumbani na kampuni imejipanga kupanua huduma zake katika mikoa mbalimbali ikiwemo Jiji la Dodoma, Arusha na Mwanza.
Kufunguliwa kwa migahawa ya kisasa ya Pizza Hut naKFC katika eneo moja katika jengo la Mikocheni Plaza, kunatoa fursa kwa wateja kupata huduma bora za chakula hususani Pizza na nyama ya kuku zinazotolewa na migahawa hiyo,inao ukubwa wa eneo la kutosha kuhudumia wateja 90 kwa wakati mmoja,menu za chakula za kidigitali,sehemu nzuri na salama za watoto kuchezea, na mazingira rafiki ya kukutana kwa chakula cha kifamilia na mijumuiko ya sherehe ndogondogo.