Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Petroli yaadimika Zanzibar!

Wamiliki Wa Magari Kenya Waingia Tanzania Kununua Mafuta Ya Bei Rahisi Petroli yaadimika Zanzibar!

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zanzibar inakabiliwa na ukosefu wa mafuta ya Petroli kwa siku mbili mfululizo na kusababisha adha kwa wananchi wanaohitaji nishati hiyo.

Tatizo hilo limeanza Aprili 14, 2024 hadi leo Aprili 16, 2024 vituo vingi vya kuuzia mafuta vimeshuhudiwa vikiwa na idadi ndogo ya wafanyakazi kinyume na ilivyozoeleka.

Kutokana na kadhia hiyo, kumesababisha kupanga kwa gharama za usafiri wa bodaboda. Mwananchi Digital imeshuhudia ongezelo la Sh1,000 zaidi kwa njia za mjini kwa mfano kutoka Michenzani hadi Malindi Mjini kwa abiria analazimika kulipa Sh3,000 baada ya Sh2,000 iliyozoeleka.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema vituo vyote vya Zanzibar vimekumbwa na changamoto hiyo, huku wakiwaomba radhi wananchi.

Kupitia taarifa yao kwa vyombo vya habari wamesema changamoto hiyo imesababishwa na kuchelewa kwa meli ya mafuta ambayo ilikwenda kupakia mafuta hayo katika Bandari ya Tanga, Tanzania na kuipeleka visiwani humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live