Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pesapal yaboresha mfumo kuharakisha usalama wa malipo

Pesapal Malipo Pesapal yaboresha mfumo kuharakisha usalama wa malipo

Tue, 4 Oct 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Pesapal, Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma ya malipo kidijitali, inayotoa huduma nchini Tanzania na Afrika Mashariki, imeboresha muonekano wa programu (Application Programming Interface) API hadi Pesapal 3.0, ili kuruhusu utoaji wa vipengele vilivyoimarishwa vya usalama pamoja na maboreshi kwa mtumiaji, mawakala na walaji katika masoko yote ambapo Pesapal inatoa huduma.

Kama sehemu ya uboreshaji wa API hadi Pesapal 3.0, Pesapal imeanzishisha huduma ya 3-D Secure kwa malipo ya kadi na kuanzisha Sim Tool Kit (STK) kwa malipo ya pesa kwa njia ya simu.

Vipengele hivi vipya vya Pesapal 3.0 vimeboresha (muonekano kwa mtumiaji) User interface na Uzoefu kwa mtumiaji (User Experience) si tu kwa watumiaji wa mwisho bali pia kwa watengenezaji wa programu. Pamoja na hayo, mabadiliko haya yanabainisha matumizi ya machaguo mengi ya uthibitishaji wa hatua za juu kuondoa matukio ya ulaghai na urejeshaji wa malipo.

Akizungumzia uboreshaji huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Pesapal, Agosta Liko alisema kutokana na ukuaji wa malipo ya biashara kidijitali kuongezeka Afrika Mashariki, Pesapal inaendelea kuwekeza katika teknolojia za kibunifu ili kuweka imani ya hali ya juu miongoni mwa watumiaji na wafanyabiashara.

"Kutokana na ukuaji wa hali ya juu kwenye biashara ya malipo kidijitali, imekuwa muhimu sana kipindi hiki kwa biashara zote kuwa na ulinzi thabiti na maboresho ya muonekano wa programu zao (API). Tumefurahishwa na aina mpya ya huduma inayotolewa kupitia Pesapal 3.0, na vipengele vipya vinatuwezesha kuleta huduma za ongezeko la thamani sokoni,” Bw. Liko alisema.

"Kwa kukidhi viwango vya kimataifa vya malipo ya kielektroniki, tunaweza kukabiliana na hatari na hivyo kuongeza Imani kwa wateja katika matumizi ya kadi za mikopo na kadi za benki au hata fedha kwa njia ya simu katika mifumo ya malipo kidijitali

3-D Secure ni itifaki ya malipo iliyoundwa ili kutoa safu ya ziada ya ulinzi ili kusaidia kuzuia ulaghai kwa kuwawezesha watumiaji kujithibitisha kwa watoa kadi zao za malipo wanapofanya ununuzi kwenye chaneli za kidijitali. Pia huwapa mawakala na watoa huduma njia ya uhakika ya kuthibitisha wamiliki wa kadi kwa miamala ya biashara kidijitali kabla ya kuwaidhinisha.

Pesapal imejitolea kutoa uzoefu wa malipo jumuishi na wa hali ya juu, kuhakikisha inatoa majibu yanayokidhi mahitaji ya kila siku ya wateja wake. Tangu 2009, Pesapal imeendelea kutoa mazingira salama ya malipo huku ikizingatia viwango vya juu zaidi vya usalama.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz