Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pato la taifa laongezeka kwa Sh trilioni 1.5

1452a7fdefb5d751e40df92248e16bfa Pato la taifa laongezeka kwa Sh trilioni 1.5

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

PATO la Taifa kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2021 limeongezeka hadi sh trilioni 38.0 kutoka sh trilioni 36.4 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2020.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Daniel Masolwa, jijini Dodoma.

“Katika kipindi cha robo ya kwanza 2021, shughuli za uchimbaji madini na mawe zimeongoza kwa kuwa na kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa asilimia 10.2, ikifuatiwa na habari na mawasiliano asilimia 9.1, uchukuzi na uhifadhi mizigo 9.0, maji safi na majitaka 9.0, huduma za kitaalam, sayansi na ufundi 7.8, huduma zinazohusiana na utawala asilimia 7.4 na umeme 7.2,” amesisitiza Masolwa

Kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu Sura 351, takwimu hizi za Pato la Taifa kwa robo ya kwanza ya mwaka 2021 ni rasmi na zinatumika katika kufuatilia na kutathmini malengo yaliyowekwa katika sekta za kiuchumi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz