Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pato la kila mtu lafikia Mil. 2.8

Mwigulu Klmn Pato la kila mtu lafikia Mil. 2.8

Thu, 15 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema mwaka 2022 Pato Ghafi la Taifa lilikuwa TZS trilioni 170.3 ikilinganishwa na TZS trilioni 156.4 mwaka 2021.

Hivyo, kutokana na idadi ya watu Tanzania Bara, Pato la Taifa kwa Mtu kwa mwaka 2022 ni TZS milioni 2.844 ikilinganishwa na TZS milioni 2.708 mwaka 2021.

Kiasi hicho ni sawa na dola za Marekani 1,229.1 mwaka 2022 kwa mtu kwa mwaka ikilinganishwa na dola za Marekani 1,173.3 mwaka 2021. Hali hii inaendelea kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ngazi ya chini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live