Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Panga la laini za simu lapitia zilizosajiliwa

94123 Laini+pic Panga la laini za simu lapitia zilizosajiliwa

Mon, 3 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Panga la uzimaji laini ambazo hazijasajiliwa kwa mfumo wa alama za vidole linaloendelea kwa zaidi ya milioni 12, limeibua malalamiko ya kuzimwa laini kadhaa licha ya kusajiliwa huku Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwataka walalamikaji kufuatilia madai yao.

Madai hayo yanajitokeza ikiwa ni siku tatu tangu kampuni za simu zilipotakiwa na TCRA kuanza kuzima laini hizo awamu ya nne.

Juzi, Naibu Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye alilieleza Bunge kuwa laini milioni 31 kati ya milioni 43 za simu zilikuwa zimesajiliwa kwa alama za vidole.

Abubakary Mohammed, dereva na mkazi wa Jiji la Dar es Salaam alisema alizimiwa laini yake juzi licha ya kusajili Septemba mwaka jana. “Niliposajili ilikuwa inatumika bila tatizo lakini niliposafiri nje ya nchi na kurudi jana (juzi) haikufanya kazi tena,” alisema.

Hata hivyo, mkuu wa kitengo cha mawasiliano kwa umma TCRA, Frederick Ntobi alisema ni hali ya kawaida kujitokeza dosari za aina hiyo katika mifumo huku akiwataka kutumia namba maalumu za kuwasilisha malalamiko kupitia kituo cha mawasiliano TCRA.

Naye mkuu wa mawasiliano Vodacom, Jacquiline Materu aliahidi jana angetoa ufafanuzi baadaye lakini hakupatikana tena.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz